Makamu mwenyekiti taifa CCM Phillip Mangula |
Makamu mwenyekiti taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Phillip Mangula amewataka viongozi wa matawi kusimamia ipasavyo kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili wa chama hicho kwa kupiga vita rushwa hasa kuelekea katika chaguzi za serikali za mitaa zinatarajiwa kufanyika mwaka huu.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika salama za mwaka wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya tawi la ofisi ndogo za chama hicho lilipo Mtaa wa Lumumba.
Amewataka viongozi hao kuweka misingi mizuri ambayo itawezesha kupatikana viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya ya rushwa ili kuwa na dira nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.
“Nataka kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili ziheshimiwe ili kupata viongozi ambao hawatatokana na rushwa, na hakikisheni katika vikao vyenu vya chama mnasimamia agenda mbili ambayo ni uchaguzi na kujadili mwenendo wa katiba mpya”
“Mkifualia hatua moja hadi nyingine katika mchakato wa kuipata katiba kuanzia ushiriki wa wajumbe wa bunge maalum hadi katika mjadala wa wajumbe wakipitia kifungu kimoja hadi kingine mtakuwa na nafasi kubwa ya kutoa maoni yenu pale itakaporudi kwa wananchi,”alisema Mangulla.
Akizungumzia uwepo wa serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya, Mangula amesema bado ni mapema mno kuzungumzia hatia ya suala hilo kwani mchakato wa kuipata katiba bado mrefu ambao mbali na wawakilishi wa bunge maalumu la katiba utashirikisha tena wananchi ambao watapiga kura yao ya mwisho. SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment