HABARI MPYA

Monday, June 22, 2015

KINANA AZUNGUMZA NA WAFANYA BIASHARA WA SOKO KUU LA SENGEREMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabishara wa Soko Kuu Sengerema mjini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia miundo mbinu ya maji taka inayolalamikiwa na wafanyabiashara wa soko kuu la Sengerema.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya miundo mbinu ya maji taka katika soko kuu la Sengerema mjini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara na vijana wa stendi ya Sengerema.    
Wafanyabiashara wa Soko Kuu Sengerema mjini wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kuwanyimannafasi ya kuendeleza eneo la Soko.
Wakizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ),  Abdulrahman Kinana kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wamelalamika kukosekana kwa maji safi na salama,miundo mbinu mibovu ya maji taka pamoja na vyoo .
Pia walilamikia kunyimwa nafasi ya kujenga vibanda vya biashara kwa madai Halmashauri inataka kujenga soko la kisasa ambalo limekuwa ahadi kwa zaidi ya mika 10 sasa.
 Wamesema wanashangaa uongozi unawanyima nafasi ya kujenga lakini viongozi haohao wanashindwa kujenga kwa madai ya kukosa fedha huku wakiendelea kukusanya ushuru kila kukicha.

No comments:

Post a Comment