HABARI MPYA

SHINA LA CCM MODENA


                  MODENA- ITALIA


Viongozi wa tawi la CCM la Napoli katika picha ya pamoja wakiwa na Mwenyekiti wa shina jipya la CCM  la Modena Ndugu Mary Julius Mtemahanji, mara baada ya kuchaguliwa  na wanachama wa CCM kushika wadhifa huo.
Tarehe 3/11/2012 itabaki katika  historia ya Chama cha Mapinduzi ughaibuni , baada ya kufunguliwa shina la kwanza nchini Italy. Ufunguzi huo ulisimamiwa na kuendeshwa na viongozi wa Tawi la Napoli ambalo ni tawi pekee nchini Italy.Wanachama wa CCM Modena  walimchagua Bi MARY  JULIUS MTEMAHANJI kuwa Mwenyekiti, baada ya mchuano mkali wa kura kati yake na ndugu PASKAL NYALUSI JONAS ambaye baadae alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya uongozi. Wengine waliochaguliwa ni Katibu wa shina ndugu MWINYIMWAKA HATIBU SARAI, bi HALIMA MWEVI, Bi SALAMA KASIBA, na Bi LEYLA  RAYMOND walichaguli kama wajumbe wa kamati ya uongozi.

Mwenyekiti wa shina la CCM la Modena-Italy   

                         ndugu Mary Julius MtemahanjiKAMATI YA UONGOZI YA SHINA
  • Mwinyimwaka Hatibu Sarai (katibu wa shina)
  • Halima Mwevi
  • Nyalusi Paskal Jonas
  • Leyla Raymond
  • Salama kasiba

No comments:

Post a Comment