Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Chiungutwa wilayani
Masasi na kuwaambia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi
awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi
alisema lazima tutangulize utumishi kwa umma.
Kadi zilizorudishwa kutoka kwa
wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na
kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani
Masasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama
cha NLD Taifa Ndugu Frank Rashid Maulano aliyejiunga na CCM kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa jimbo la
Lulindi wilayani Masasi.
Wanachama wapya waliojiunga na CCM
pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo
cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo
alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya
Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Wananchi wa Kijiji cha Machombe
wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima
kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu
Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la
maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani wakati wa
kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Marika wilayani Masasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Marika
ikiwa sehemu ya kujenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Chiungutwa jimbo
la Lulindi wilayani Masasi ambapo alikagua maendeleo ya mradi wa maji wa
Chiungutwa mradi ambao utasaidia vijiji 27,tarafa 3 ambapo watu zaidi
ya elfu 60 watanufaika na mradi huo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa wilaya ya
Masasi ambapo aliwapongeza kwa kutambua utapeli wa vyama vya upinzani
katika kijiji chao na kuamua kujitenga nao kabisa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa ambapo
aliwapongeza kwa kuwa na Mbunge mchapa kazi anayejali wananchii
wake,Kinana aliwaambia wananchi hao wahakikishe wanajiandikisha tayari
kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Mbunge wa Jimbo la Lulindi ( CCM ) Jerome
Bwanausi akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa na kuwaeleza
maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwenye jimbo lake wakati wa
mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mbunge wa zamani wa mkoa wa
Mtwara John Aidi aliyekuwa mbunge wa Mtwara miaka ya 75 mpaka 85 na
aliwahi kuwa mbunge wa Masasi miaka ya 65 mpaka 70 akifuatilia kwa
makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
No comments:
Post a Comment