HABARI MPYA

Friday, September 28, 2012

TAWI LA CCM NAPOLI ITALY

Pichani baadhi ya wajumbe na viongozi wa tawi.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya tawi la Napoli, walikutana siku ya tarehe 21/09/2012. Kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa tawi ndugu Abdulrahamani A.Alli kilijadili mambo kumi muhimu.Katika kikao hicho  wajumbe walijadili mengi yanayohusu changamoto za kisiasa na maendeleo katika tawi. Halmashauri kuu ya CCM ya tawi itakutana tena siku ya tarehe 05/10/2012, tarehe iliyopangwa na kikao cha Sekretarieri ya halmashauri kuu ya CCM ya tawi  kilichofanyika siku ya  jumatano ya tarehe 26/09/2012. Kikao  cha sekretarieti ya halmashauri kuu ya CCM ya tawi kilipanga na kufanya marekebisho ya tarehe za vikao vya tawi kwa kumalizia mwaka 2012.( picha na B.Millinga(Mjumbe)

No comments:

Post a Comment