HABARI MPYA

Thursday, March 31, 2011

TAWI LA CCM NAPOLI LATIMIZA MWAKA MMOJA








Jana tarehe 25/03/2011 tawi la CCM Napoli -Italy limetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa rasmi.
Sherehe ya kutimiza mwaka iliambatana na ufunguzi wa Club ya CCM. Mwenyekiti wa tawi katika hotuba fupi ya kuadhimisha mwaka mmoja alielezea kwa kifupi mafanikio ya tawi na malengo ya baadae. pia mwenyekiti alisema ufunguzi wa mashina  ya CCM  unasubiri kupangwa kawa tarehe na wanachama wote watatangaziwa rasmi ili kuweza kuhudhuria ufunguzi huo.
 Mwenyekiti aliwataka Watanzania wote kujisikia wako nyumbani na kuwa club ni ya CCM lakini ipo kwa watanzania wote. meneja wa Club hiyo ndugu Abdulwahab Mohamed alisema club hapo patapatikana chakula pamoja na vinywaji,pia kwa wapenzi wa soka watakuwa wakiburudika na ligi kuu ya Italy,champions  na mashindano mengine.pia kwa wale watakopenda kuutumia ukumbi huo kwa ajili ya sherehe za birthday nk wanakaribishwa.

No comments:

Post a Comment