HABARI MPYA

Sunday, November 7, 2010

CCM TAWI LA NAPOLI LASHEREHEKEA USHINDI

Pichani ni Viongozi wa tawi la CCM Napoli pamoja na wajumbe na baaadhi ya wadau
(picha na George Mayaka)

Usiku wa kuamkia leo jijini Napoli palikuwa hapatoshi katika mnuso  ulioandaliawa na tawi la Chama Cha Mapinduzi Napoli-Italy, sherehe hiyo iliyoalika Watanzania wote na wageni wataliani ilianza majira ya saa kumi jioni mpaka kuche.Katibu wa tawi ndugu Kagutta N.Maulidi katika salaam fupi kabla hajamkaribisha mwenyekiti wa tawi la CCM Napoli alisema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi ni wa Watanzania wote kwani ni Watanzania walioamua kuchagua tena CCM kuliongoza taifa letu.Aidha katibu aliwataka watanzania kuendeleza umoja wao na ushirikiano.  Mweyekiti wa tawi ndugu Abdulrahaman A.Alli wakati wa kufungua sherehe hiyo aliwashukuru na kuwapongeza Watanzania wote,wana usalama, wasimamizi wa uchaguzi wote na serikali kwa jumla kwa kuendesha uchaguzi wa amani,   wengi wa wageni wataliani waliokuja katika sherehe walikuwa wametokea Tanzania kwa utalii, wamesifia sana usalama na amani ya Tanzania.
Aidha mwenyekiti alimpongeza Mh Raisi Dr JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa kuchaguliwa tena kuliongoza taifa letu.Katika sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa jumuiya ya Watanzania Italy tawi la Modena,Padova,Genova ,Mwakilishi wa Jumuiya ya Wanzania Italia TANZANIA ndugu EMANUEL KAPONGO na  Wanajumuiya wanaoishi Roma. Usiku wa jana watanzania wengi waliomba fomu za kujiunga na Chama cha Mapinduzi.(picha za tukio tembelea WABONGO UGHAIBUNI)

No comments:

Post a Comment