HABARI MPYA

Tuesday, September 2, 2014

UK: MKUTANO MKUU WA CCM

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM UK Ndugu Maina Owino (Left) akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti Mpya CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma.
Mkutano mkuu wa wanachama wote CCM UK ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM UK umefanyika katika jiji la Reading siku ya Jumamosi tarehe 30/08/2014 ambapo wagombea watatu walipitishwa na vikao vya awali kugombea nafasi hiyo ni Ndugu Said Surur, Peter Gabagambi na Kapinga Kangoma na kujaa shamrashamra na nderemo na  kuhudhuriwa na wanachama wa CCM UK NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA pia viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM aliyeng”atuka Ndg  Maina Ang’iela Owino, Makamu Mwenyekiti  Ndugu Said Sukwa, Kaimu Katibu Ndugu Leybab Mdegela,  Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu Mohamed Upete, Viongozi wa mashina, wajumbe na wanaCCM toka mashina ya CCM UK.
Mkutano huo ulianza kwa  Katibu mwenezi ndugu Abraham Sangiwa kuwashukuru Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi hapa UK ili kuleta chachu ya mabadiliko ndani na nje ya chama kwa manufaa ya watanzania wote kwa ujumla.
Ndg Sangiwa aliwakumbusha kuwa kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.
Akimkaribisha Mwenyekiti mstaafu Ndugu Maina A Owino, Kaimu Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela aliwashukuru wanachama wote kwa kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha malengo ya mkutano huo na zoezi la kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM UK na kuwafahamisha wanachama wagombea wawili Ndugu Said Surur na Peter Gabagambi waliopitishwa na vikao vya awali wamejitoa katika kinyanganyiro hicho hivyo mgombea pekee aliyebaki katika nafasi hiyo ni Ndugu Kapinga Kangoma, pia ripoti ya Tawi iliwakilishwa na itasambazwa na viongozi wa mashina kwa wanachama wote.
SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment