pichani kutoka kushoto ni katibu wa tawi ndugu Kagutta N.Maulidi, Mwenyekiti wa tawi,ndugu Abdulrahaman A.Alli, katibu siasa (mwenezi) ndugu Allan Bendera na mwisho ni katibu uchumi mama Fatuma A.Tandika.
Tarehe 25/03/2010 ni siku iliyoingia katika historia ya CCM baada ya kuanzishwa tawi jipya la Chama cha Mapinduzi mjini Napoli. Viongozi hao wa tawi wanategemea kukutana tena mapema April kwa ajili ya kupeana majukumu. Mwenyekiti amewataka wale wote ambao walichelewa kurudisha fomu za maombi ya kujiunga na CCM kuwasiliana na katibu wa tawi.
No comments:
Post a Comment