HABARI MPYA

Monday, July 7, 2014

PONGEZI MWENYEKITI CCM-UK

Mwenyekiti -Maina Ang'iela Owino
Wanachama wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Uingereza wanategemea kufanya uchaguzi ,kujaza nafasi ya uongozi (mwenyekiti) iliyoacha wazi na Mwenyekiti wa tawi hilo ndugu Maina Ang'iela Owino,aliyeshikilia nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa tawi la CCM -UK.

Sijapata kumuuliza ndugu Owino sababu za kung'atuka kwake,lakini naamini amefanya hivyo kwa nia njema kabisa. Lakini pia naweza kuhisi labda ni kuzidiwa na majukumu na pia kutoa nafasi kwa wanachama wa tawi kuchagua kada mwingine kwani naamini kwa uongozi wake tayari kuna wanachama wengi wamesha komaa na wanaweza kushika nafasi hiyo bila ya wasiwasi.

Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza ndugu Owino kwa uamuzi wake ambao unaonyesha kukomaa kisiasa na kiuongozi. Naamini kuwa atakuwa pamoja na uongozi mzima wa tawi na wanachama kwa jumla kuhakikisha tawi linasonga mbele zaidi.


Elewa kuwa Chama bado kinahitaji wanachama wenye moyo kama wewe wa kukitumia chama ,wanachama na nchi kwa jumla

Tunawatakia  kila heri katika mchakato mzima wa kumpata kada atakayeshika nafasi hiyo ya mwenyekiti.  KIDUMU CHA CHA MAPINDUZI!!!

Kagutta N.Maulidi
katibu wa tawi
CCM-Italy.